Monday, April 03, 2006

Karibuni mabibi na mabwana!

Wasomaji wapendwa - Nimetiwa moyo kuanza kublogu katika Kiswahili na kumbukumbu niliyo nayo kwa heshima ya waalimu wangu wa Kiswahili nilokuwa nao tangu darasa la kwanza hadi shule ya upili. Hivi namshukuru marehemu Bi. Rose Okello, Bi. Akoto, Bw. Obed, Bw. Misiko na Bi. Maloba. Kidogo nilikaribia kuupoteza ubingwa walonipa hao mabibi na mabwana nilipoelekea chuo kikuu nchini Kenya na Marekani, walakin kazi yangu ya uandishi habari ilizidi kunikumbusha kitambo kile kitamu:-) Pia nawashukuru marafiki zangu toka Kenya na Tanzania ambao, kwa bidii yao katika kutunza usanifu wa lugha hii tukufu, wamenitia moyo kuzingatia mwendo huu. Mwisho, nawashukuru wazee wangu ambao - tofauti kabisa na Wakenya wengi - wazingatia umuhimu wa kuzungumza na kuandika Kiswahili sanifu. Blogu hii itawapeni habari zote nitakazochapisha kwenye ile blogu yangu ya Kiingereza, yaani Kenyananalyst. Ni matumaini yangu kuwa sitowanyimeni ukweli na utamu mnaostahili kwa kuwa wasomaji wangu waaminifu katika lugha hii "mpya" namna mlivyokuwa upande wa pili. Karibuni tena na Mungu awabariki! Mwenzenu, Yesse.

0 Comments:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home